Rc Makonda : Tusinyooshe vidole kifo cha Akwilina - MSUMBA NEWS BLOG

Thursday, 22 February 2018

Rc Makonda : Tusinyooshe vidole kifo cha Akwilina


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewataka wananchi kuacha kunyooshea vidole na kurushia lawama juu ya kifo cha mwanafunzi Akwelina Akwilin kwani Jeshi la Polisi linaendelea kufanya uchunguzi wake na watakapomaliza watatoa taarifa kamili
Makonda ameeleza hayo wakati aliposhiriki katika ghafla ya kuaga mwili wa marehemu Akwelina katika chuo cha Taifa cha Usafrishaji (NIT) ili aende kupumzishwa kwenye nyumba yake ya milele huko Mkoani Kilimanjaro.
"Jeshi hili la Polisi litatupatia majibu watakapomaliza kazi yake, ombi langu kwenu wananchi wa Dar es Salaam hasa wale ambao hatujawahi kusomea mambo ya uchunguzi na wala hatuyajui tusiwe wa kwanza kunyoosha vidole na kuhukumu kabla hatuja hukumiwa. Mimi najua mtoa hukumu wa kweli ni Mungu na anazo siri zote kwa nini Akwilina ameondoka tarehe 16", amesema Makonda.
Pamoja na hayo, Makonda ameendelea kwa kusema "naendelea kuwasihi tuwape nafasi wenye majukumu yao watimize kazi yao na hatimae na sisi tuunganike mkoa kama taifa kuhakikisha amani inatawala katika mkoa wetu kwa kila mtu".
Kwa upande mwingine, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ameitaka familia ya marehemu Akwelina iwe yenye uvumilivu katika kipindi kigumu walichonacho kwa sasa.
Comments


EmoticonEmoticon

Notification
This is just an example, you can fill it later with your own note.
Done