Thursday, 22 February 2018

Mwili wa Akwilina waagwa rasmi


Mwili wa mwanafunzi aliyepigwa risasi na askari polisi siku ya Ijumaa, Februari 16, Akwilina Akwilini, umeagwa rasmi leo na maelfu ya waombolezaji pamoja na wanafunzi wa chuo cha Usafirishaji, na kisha kuanza safari kuelekea mkoani Kilimanjaro kwa ma
Shughuli ya kuaga mwili huo imefanyika mchana huu katika vianja vya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), huku pia baadhi ya viongozi mbali mbali wa serikali na watu maarufu wakihudhuria tukio hilo, lililowaacha mamia na machozi ya kumlilia mpendwa wao.
Miongoni mwa waliohudhuria ibada hiyo ni Waziri wa Elimu Joyce Ndalichako, Kamanda wa Polisi Kanda maalum Dar es salaam Lazaro Mambosasa, Msanii Bill Nas, John Mnyika, Salum Mwalimu na wengineo ambao ilikuwa ngumu kuwatambua kutokana na wingi wa watu.
Baada ya Ibada hiyo mwili wa Akwilina ulichukuliwa na kuingizwa kwenye gari maalum tayari kwa kuanza safari, huku ndugu, jamaa na marafiki wakitumia magari ambayo yalikuwepo uwanjani hapo, nhuku wengine wakitakiwa kulipia elfu 40 kwa ajili ya nauli ya kwenda na kurudi mkoani Kilimanjaro
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: