Chloe Kim
Kumpongeza mtu yeyote yule sio jambo mbaya lakini linapokuja suala la kumpongeza hadi kupita mipaka huenda watu wakapata tafsiri tofauti na kuibua hisia mbaya hii imemtokea mtangazaji wa kituo cha Radio cha KNBR-AM, Patrick Connor baada ya kutoa pongezi zilizopelekea kufukuzwa kazi.
Bw. Connor (43) alimpongeza redioni mshindi wa Snowboarder, Chloe Kim (17) kwa kuibuka na medali ya dhahabu kwenye michuano ya olimpiki inayoendelea mjini PyeongChang, Korea Kusini kwa kumwambia kuwa ni mrembo na amejaaliwa umbo zuri.
Connor alisikika redioni akisema kuwa Aprili 23 mwaka huu itakuwa siku yake ya kuzaliwa atafikisha miaka 18 huku akidai kuwa hataogopa kumsifia uzuri wake na ndio sababu inayomfanya awapende wasichana.
Tarehe 23 Aprili mwaka huu ni siku yake ya kuzaliwa nadhani sitaogopa tena kumsifia hewani mtoto mrembo kama huyu, naanza kuhesabu siku kuanzia leo,“amesema Connor huku akiendelea kumpamba msichana huyo hewani.
Ndio maana huwa napenda sana wasichana wa sekondari, kama angekuwa amefikisha miaka 18 leo hii ningemsifia uzuri wake wote, hata hivyo sisiti kumsifia msichana huyu mrembo mwenye umbo zuri, Oooo My God!!“amemaliza Connor.
Baada ya kauli hiyo hewani wasikilizaji walianza kuporomosha maoni yenye matusi kwa kituo hicho cha habari wengi wakisema mtangazaji huyo ametoa maoni ya kudhalilisha watoto kingono redioni.
Hata hivyo, baada ya kupata malalamiko mengi pamoja na kutukanwa Patrick Connor alienda kwenye mtandao wa Twitter na kuwaomba radhi wamarekani wote huku akidai kuwa alikusudia kuuchekesha umma na sio kama ilivyopokelewa.

Tayari uongozi wa kituo hicho cha redio kupitia mtandao wao wa KNBR.COMumeshatangaza kuwa umemfukuza na kutangaza nafasi moja ya kazi kuziba pengo hilo.
Chanzo:The Independent
Share To:

msumbanews

Post A Comment: