Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amefunguka na kuwashauri wanaume wenzake kuacha kuwa na mahusiano na wanawake wasiokuwa na mawazo ya kupambana na hali ya uchumi wa maisha na badala yake kutaka kula starehe peke yake bila ya kujali kesho yao
Gambo ametoa nasaha hiyo katika ukurasa wake maalumu wa kijamii baada ya kuwepo rundo la wanawake ambao kazi yao kubwa ni kutafuna pesa za wanaume waliokuwa nao katika starehe nasio kuwashauri ni namna gani wafanye wajikwamue katika maisha hasa ya sasa ambayo wengi wao wanasema yamekuwa magumu.
"Mwanaume Kama unania ya dhati kuwa na 'economic freedom in this tough economy' basi inatakiwa uepukane na wale wanawake aina ya 'Babe' nina njaa, nibebee Pizza au Chips kuku usisahau kuweka 'mayonaise' au 'Babe' simu Iphone X imetoka naomba ninunulie", amesema Gambo.
Pamoja na hayo, Gambo ameendelea kwa kusema "achana na huo ujuha badala yake pata mwanamke aina ya 'Babe' umekula au unataka nikupikie chakula gani leo, au 'Babe' ni nini 'future' yako naona hujaweka vizuri vipaumbele vyako. Spidi ya mwanaume kuwa na maendeleo na hatimae kushinda uhuru wa kiuchumi inategemeana sana na aina ya mwanamke uliyenae. Mwanamke bora ni uwekezaji wenye faida kubwa na mwanamke asiejua nafasi yake ni mzigo na 'liability' kubwa sana".
Kwa upande mwingine, Gambo amesema endapo pale mtu akipata maendeleo basi asiwe mbahili wala asisahau kufurahia na mwanamke aliyekuwa nyuma ya mafanikio yake
Share To:

msumbanews

Post A Comment: