MREMA adai Mtulia wa ccm ni Kunguru asiyefugika asichaguliwe


Mwenyekiti Wa chama cha Siasa cha TLP,Agustino Lyatonga Mrema amemfananisha mgombea ubunge Wa Ccm katika jimbo la Kinondoni ,Maulid Mtulia na kunguru kutokana na tabia zake za kuhama ovyo na kuwataka wananchi wasimchague kwa sababu ameonyesha dalili za kutokuwa mwaminifu asije kuwaacha kwenye Mataa.

Mrema ameyasema hayo ikiwa ni siku moja kabla ya wananchi kufanya uchaguzi Wa ubunge hapo kesho Jumamosi,Feb 17 mwaka huu.

Amewatahadharisha wananchi kwamba watajutia muda wao walioupoteza kwenye kampeni kwani Mtulia  si MTU sahihi Wa kuwaondolea kero zao Bali ni MTU anayesaka maslahi binafsi ikiwemo kufanyabiashara ya ubunge.

Aidha amewataka wananchi wa jimbo hilo kumchangua mgombea wake kupitia chama cha TLP ,Dr.JOFREY MALISA akijipambanua kuwa ni Kijana msomi aliyebobea  katika masuala ya uongozi.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: