Saturday, 24 February 2018

Mourinho: Jiandaeni na burudani Old Trafford

Kocha wa Manchester United Jose Mourinho, amesema mashabiki wajiandae na burudani kwenye uwanja wa nyumbani wa Old Trafford, ambapo timu hiyo itacheza mechi nne nyumbani.

Akiongelea mchezo wa kesho dhidi ya Chelsea Mourinho amesema ana imani huo ni mchezo wa kwanza kati ya michezo mingine ambayo watacheza nyumbani ndani ya mwezi huu na Machi hivyo hana shaka kuwa watatumia vizuri uwanja wao.

"Nadhani wiki chache zijazo Old Trafford itashangaza, tuna mechi mbili kubwa za ligi, tutafanya vizuri dhidi ya Chelsea na Liverpool pamoja na mechi yetu ya ligi ya Mabingwa," amesema.

Baada ya mchezo wa kesho dhidi ya Chelsea vijana wa Mourinho wataanza mwezi Machi na safari ya kwenda kucheza na Crystal Palace kabla ya kuwakaribisha Liverpool.

Baada ya hapo United itakuwa mwenyeji wa Sevilla kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa hatua 16 kabla ya kucheza robo fainali ya Kombe la FA dhidi ya Brighton. Man United kwasasa inashika nafasi ya pili ikiwa na alama 56.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: