Monday, 12 February 2018

Mh. Zitto amjulia hali Mbwana Samatta UbelgijiKiongozi wa Chama cha ACT – Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amesema kuwa jana jioni alikwenda Genk nchini Ubelgiji nyumbani kwa nyumbani kwa Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars Mbwana Ally Samatta.
Zitto amesema kuwa amefurahi kumsalimia na kumjulia hali Samatta huku akieleza kuwa amefurahi kumkuta akiwa mzima wa afya.
Nimepita Kumsabahi Nahodha Samatta – Zitto
Jana jioni nilikwenda Genk, hapa Ubelgiji, nyumbani kwa Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, ndugu Mbwana Ally Samatta, ambaye ni mchezaji wa Klabu ya KRC GENK inayoshiriki Ligi Kuu ya hapa Ubelgiji.
Nimefurahi kupita kumsalimu na kumjua hali Samatta, nimefurahi zaidi kumkuta akiwa ni mzima wa afya na anashiriki mazoezi ya timu yake bila shida. Inatia moyo zaidi kuona Kijana huyu mwenzetu wa Kitanzania namna anavyofanya kazi kwa bidii ili aweze kufanikiwa zaidi.
Namuomba Mola amuwezeshe kutimiza ndoto zake.
Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo
Genk
Ubelgiji
Februari 13, 2018
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: