Lionel Messi na Andres Iniesta
Mshambuliaji wa klabu ya Barcelona, Lionel Messi jana usiku amefanikiwa kuiokoa klabu yake kutoka kwenye kipigo kwa kuisawazishia goli 1-1 dhidi ya mabingwa wa Uingereza Chelsea kwenye mchezo wa klabu bingwa barani Ulaya.
Goli hilo la kusawazisha la Messi limevunja rekodi mbovu ya mchezaji huyo ya kutofunga goli lolote dhidi ya Chelsea pindi timu hizo zinapokutana akiwa na timu yake kwa zaidi ya miaka 7.
Imemchukua mchezaji  huyo dakika 730 na mechi 9 kufunga bao lake la kwanza katika michuano ya Klabu Bingwa Barani Ulaya (UEFA).
Messi ambaye amekuwa yuko katika kikosi kimoja na Andres Iniesta tangu aanze kuichezea Barcelona mpaka sasa, alikuwa hajawahi kuzigusa nyavu za Chelsea, hadi Jana usiku ilipomlazimu kutumia dakika 75 uwanjani kupata goli hilo.
Iniesta ndiye aliyemsaidia Messi kufunga bao hilo kwa pasi safi ya mwisho kunako dimba la Stamford Bridge.
Goli la Chelsea lilifungwa na Willian kunako dakika ya 62 kwa shuti zuri lililopita miguuni mwa mabeki wa Barcelona.
Kwa sare hiyo Barcelona imekuwa na faida ya goli moja la ugenini, kabla timu hizo hazijakutana tena katika mchezo wa marudiano utakaochezwa kwenye Uwanja wa Camp Nou, Jumatano ya March 14 2018
Share To:

msumbanews

Post A Comment: