Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema apigwa kalenda


Ushahidi wa video katika kesi ya uchochezi inayomkabili Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema uamuzi umeahirishwa kutolewa leo katika Mahakama ya Wilaya Arusha. 

Akitoa sababu za kukwama kutolewa kwa uamuzi huo, Hakimu Chrisanta Chitanda, amesema anaiahirisha kesi hiyo hadi Machi 23 mwaka huu kutokana na hakimu anayesimamia kesi hiyo hayupo.

“Hakimu anayesikiliza kesi hiyo, Devotha Msofe, hayupo leo na hivyo naiahirisha hadi atakapokuwepo, Machi 23, mwaka huu,” amesema.

Awali ushahidi huo ulishindwa kuwasilishwa mahakamani hapo Januari 23 mwaka huu, baada ya upande wa utetezi kupinga kuwasilishwa mahakamani hapo sababu shahidi huyo siye aliyeandaa.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 komentar: