MBUNGE LEMA ASAHAU NAFASI YA UBUNGE 2020 JIMBO LA ARUSHA MJINI - MSUMBA NEWS BLOG

Tuesday, 20 February 2018

MBUNGE LEMA ASAHAU NAFASI YA UBUNGE 2020 JIMBO LA ARUSHA MJINI


Katibu wa CCM Wilaya ya Arusha Mjini Bwana Mussa Matoroka amefunguka na kusema kuwa Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema (CHADEMA) Asahau nafasi yake ya ubunge mwaka 2020 kwa kuwa hakuna mwananchi atakayemchangua tena.

Akizungumza na Kusaga News Ofisini Kwake matoroka amesema kuwa wananchi wa jimbo la Arusha mjini tayari wameshajielewa na wanajutia ni kwanini walimchagua mbunge huyo ambaye hana muda na wananchi wake waliomchagua.

Ameongeza kuwa serikali ya awamu ya Tano chini ya Raisi Magufuli  imejikita katika kutatua shida za wananchi maskini ndiyo maana kauli ya Hapa Kazi Tu na ilani ya chama cha mapinduzi wananchi wameshaielewa.

Matoroka amesisitiza kuwa wananchi wamekuwa wakimlalamikia mbunge wao kwasababu mara nyingi hayupo jimboni kwake kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi na kwenda kuwasemea Bungeni.

“Kweli tunapotembea kwenye kata huyo ndugu mwandishi tunaona na wananchi wanasema hawamuoni Mbunge wao tangu wampigie kura unasikia tu mbunge yuko huko dar ,Kinondoni ,huko siha sasa nauliza kwani alichaguliwa huko au Arusha sasa nasema ilani ya Ccm imeleweka sana sasa Lema asahau nafasi ya ubunge mwaka 2020 na siyo Arusha Tu hata nje ya Arusha”Alisema Matoroka

Pamoja na hayo amesema kuwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2019 watashinda mitaa yote ambayoimechukuliwa na upinzani kwasababu wananchi wameielewa ilani ya chama cha mapinduzi.

Amesisitiza kuwa bado wananchi wengi walioko upinzani wanaomba kujiunga na chama cha mapinduzi na muda ukifika watasema lakini kwasasa bado wanaendelea kuwa karibu na wananchi na kutatua shida zao.
Comments


EmoticonEmoticon

Notification
This is just an example, you can fill it later with your own note.
Done