Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Al Haji Mussa Salimu amemjibu mwanadada mkosoaji wa mtandaoni Mange Kimambi kwa kudai kuwa huu ndiyo mwaka wake wa mwisho kutumia mikono pamoja na ulimi wake kutukana watu.
Sheikh huyo amesema kwamba kutokana na kitendo hicho cha Mwanadada huyo kumuanika mtandaoni na kumtolea maneno machafu yeye kama kiongozi wa dini atarudi kwenda kushtaki katika mahakama ya mbinguni ambayo haina rushwa.
Kauli hiyo ya Sheikh Mkuu imekuja ikiwa ni siku moja tangu ianze kusambaa picha yake mitandaoni na kuanza kutuhumiwa kuwa anashiriki katika kampeni za uchaguzi mdogo kukisaidia Chama Cha Mapinduzi
"Tutarejea katika mahakama ya mbinguni kwani mahakama ya Mwenyezi Mungu haina rushwa na tutamuuliza  Mwenyezi Mungu kama alimpa Huyu Mange Kimambi ulimpa mikono kwa ajilli ya kudhalilisha na kuvunja heshma za watu. Amekuwa akiwatukana viongozi wa serikali lakini kwa hekima zao wamemnyamazia kimya" Al Haji Mussa Salimu .
Ameongeza kwamba "Tunamuonya acheze na namba nyingine lakini siyo viongozi wa dini kwani wao wana mahakama ya kushatakia. Huu utakuwa mwaka wake wa mwisho kutumia ulimi au mikono yake kudhalilisha watu".
Hata hivyo Sheikh huyo amesema kwamba wapo watu wengi waliompa rai ya kutomjibu Mange Kimambi  na kwamba kumjibu kwake kutamfanya atukanwe sana laki amesema kwamba mwanadada huyo aendelee kutukana kwani dua ya mwenye kudhulumiwa haina kizuizi na kama anaishi hapa duniani basi afahamu kwamba hataendelea kuwa salama na amejihalalishia mwenyewe kwa ulimi wake na mikono yake.
Share To:

Post A Comment: