Kurudiana na Diva siwezi – Heri MuzikiMsanii Heri amesema hawezi kurudiana na aliyekuwa mpenzi wake, Diva baada ya kuzinguana hivi karibuni.
Muimbaji huyo amesema baada ya kuachana na Diva ndio itakuwa mwisho wa yeye kuingia katika mahusiano na mtu maarufu.
“Sikuwa nime-date na mtu maarufu before, wakwanza ni yeye, kwa hiyo baada yaku-date naye imekuwa ni experience kwangu, after that nisingependa ku-date na mtu maarufu.” Heri Muziki ameiambia Bongo5.
“Kurudiana na Diva siwezi, nafikiri hata yeye mwenyewe hawezi kurudiana na mimi, kwa hiyo tunaweza kumake peace hata kama hatutakuwa marafiki kila mtu anaendelea na maisha yake,” ameongeza.
Wawili hao mara baada ya kupishana na kuamua kuachana kulipelekea Diva kutoa sauti ya Heri Muziki katika wimbo ‘Waambie’ ambao Heri alifanya kwa kushirikiana na Mr. Paul pamoja na Mwana FA na Diva kuweka sauti pale alipoondoa sauti ya Heri Muziki ingawa wimbo huo ulishatoka awali.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 komentar: