Kidoti kinampagawisha Jokate


MWANAMITINDO na Kaimu Katibu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UV-CCM), Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ amefunguka kuwa kidoti chake huwa kinampagawisha.

Akizungumza na Mwandishi wetu Jokate alisema kuwa, kila mwanadamu kuna kitu anakipenda kwenye mwili wake na kwa upande wake yeye anakizimia kidoti chake kwa sababu ndicho utambulisho wake.

“Kila ninapoamka asubuhi, lazima nikichungulie kidoti changu kama kipo au kimepungua maana ndicho utambulisho wangu,” alisema Jokate.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 komentar: