Mlinzi wa pembeni wa kikosi cha Simba, Shomari Kapombe hayupo katika kikosi kitakachocheza na Gendarmerie Tnale kwenye mchezo wa marudiano wa kombe la Shirikisho barani Afrika.

Hakuna sababu yoyote ambayo imewekwa wazi kuhusu kukosekana huko kwa Kapombe lakini pia hata John Bocco ambaye alifunga mabao mawili kwenye mchezo wa kwanza naye hajapangwa kutokana na kutokuwa fit kwa asilimia 100.

Kadhalika kipa Aishi Manula ambaye aliteguka mkono wake, amepangwa kuanza baada ya ripoti ya daktari wa Simba kusema kuwa majeraha yake hayakuwa makubwa kiasi cha kumfanya kushindwa kucheza kwenye mchezo huo unaopigwa jioni hii.

Kinachoanza: Aishi Manula, Nicholas Gyan, Juuko Murushid,.Asante Kwasi, Yusuph Mlipili, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, James Kotei, Mzamiru Yassin, Emmanuel Okwi na Shiza Kichuya.

Benchi: Emmanuel Mseja, Mohamed Hussein, Mwinyi Kazimoto, Moses Kitandu, Paul Bukaba, Ally Shomari na Said Hamis Ndemla.

Waamuzi wa mchezo huo ambao utafanyika kwenye uwanja Stade du Ville nchini Djibouti wanatoka Burundi na Kamishna wa mchezo atatokea nchini Rwanda.


Mwamuzi wa kati ni Eric Manirakiza akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Pascal Ndimunzigo, mwamuzi msaidizi namba mbili Willy Habimana, mwamuzi wa akiba Pacifique Ndabihawenimana na kamishna Gaspard Kayijuka.

Matokeo ya awali 

Ikumbukwe katika mchezo wa duru ya kwanza uliopigwa jijini Dar es Salaam Simba waliibuka na ushindi mnono wa mabao 4-0 mabao ambayo yalifungwa na John Bocco, Said Ndemla na Emmanuel Okwi.

Kwa mantiki hiyo Simba wanahitaji ushindi wa aina yoyote au sare ili kujihakikishia nafasi ya kutinga hatua nyingine ya michuano hiyo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: