Shirikisho la mpira wa miguu Afrika (CAF) limewapanga waamuzi kutoka nchini Afrika Kusini kuchezesha mchezo wa Kombe la Shirikisho barani Afrika wakati Simba itakapocheza na Al Masry ya Misri Machi 7, 2018 uwanja wa Taifa saa 10:00 jioni.

Mwamuzi wa kati atakuwa Thando Helpus Ndzandzeka akisaidiwa na Zakhele Thusi Siwena mwamuzi msaidizi namba moja na Athenkosi Ndongeni mwamuzi msaidizi namba mbili wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Christopher Harrison na kamishna wa mchezo huo Tuccu Guish Chrbremedhin kutoka Eritrea.

Mchezo wa marudiano utachezwa huko Port Said Machi 17, 2018 utachezeshwa na waamuzi kutoka Eritrea.

Mwamuzi wa kati atakuwa Yonas Zekarias Ghetre akisaidiwa na Angesom Ogbamarian mwamuzi msaidizi namba moja na Yohannes Tewelde Ghebreslase mwamuzi msaidizi namba mbili wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Yemane Asfaha Gebremedhin na kamishna wa mechi hiyo atatoka Libya Gamal Salem Embaia.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: