Friday, 16 February 2018

"Hatua zinachukuliwa kwa wapinzani tu" – Mlinga


Mbunge wa jimbo la Ulanga kupitia CCM Goodluck Mlinga, amesema kwamba tabia ya kuchukuliana hatua pale mbunge anapomsema vibaya kiongozi mkubwa, haiko kwa wabunge wa CCM isipokuwa kwa upinzani ndiyo hawawezi sema ukweli watachukuliwa hatua na viongoz

Akizungumza kwenye kipindi cha East Africa Breakfast kinachorushwa na East Africa Radio, Mlinga amesema wao kama chama wanakosoana na hakuna anayechukuliwa hatua, isipokuwa vyama vya upinzani ndio wana tabia ya kuchukuliana hatua pale mbunge anapoongoea ukweli kuhusu chama, akimtolea mfano Zitto Kabwe wakati akiwa CHADEMA.

“CCM hakuna hiko kitu kwamba ukisema utaitwa kwenye kikao, hivyo vitu nenda vyama kama CHADEMA au ACT huko, CCM hamna hiko kitu, nishawahi kurusha mawe, nishawahi kusema Mheshimiwa Rais uliposhika ni pabaya, sikuwahi kupigiwa hata simu na tukikutana tunagonga tano kama kawaida, CCM hakuna hiko kitu, chama chetu sisi tunapelekeana moto kama kawaida”, amesema Mlinga.

Mbunge huyo ambaye anatokea jimbo la Ulanga ameeendelea kwa kusema kwamba wao kama wawakilishi wa wananchi lazima waongee ukweli, na kuna muda 
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: