Hapa hakuna mapenzi, kuna kazi tu – Snura

Msanii wa muziki Bongo, Snura amefunguka ukweli wa ukaribu wake na Minu Calypto.

Kumekuwa na taarifa mbali mbali kuwa Snura anatoka kimapenzi na Minu Calypto ambaye pia ni msanii wa Bongo Flava. Snura amesema kinachoendelea kati yake ni muimbaji huyo ni masuala ya kazi na hakuna kitu kingine.
Ameendelea kwa kusema picha zilizooneka wakipeana mabusu ya moto zimetoka kwa bahati mbaya ila siku ambayo kazi husika itatoka ndio watu watajua ukweli wa suala hilo.
“Hapa hakuna mapenzi kuna kazi tu, hamjui kwanini nimejitoa kumsaidia na kumsaidia mtu sio mpaka awe bwanaako ubinafsi huo mimi sina na kwakua nimejitolea kumsaidia basi nakubaliana na kuvumilia yote, huyu ni mdogo wangu na atabaki kua hivyo,” amesema.
Siku za nyuma kuliripotiwa kuwa Snura amemchukua Minu Calypto ambaye mwanzoni alikuwa ni mpenzi wa muigizaji Nisha kitu ambacho Snura alikipiga vikali.
Kwa sasa Minu Calypto anatamba na ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la Bado Nachechemea.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 komentar: