Halmashauri zapewa wiki moja


Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi ametoa muda wa wiki moja kwa Halmashauri zote katika Mkoa huo kuhakikisha zinapata na kusambaza sumu na mabomba ya kuulia wadudu wanaoshambulia zao la Pamba
Dkt. Nchimbi ametoa kauli hiyo wilayani Iramba kufuatia wakulima kulalamikia suala la ukosefu wa dawa na mabomba ya kupulizia sumu ya kuua wadudu wanaoshambulia zao la Pamba.
Aidha Dkt. Nchimbi amewataka wahusika wa kilimo katika halmashauri hizo kutoa elimu ya zao la pamba katika maeneo yote ya wakulima ili kuwasaidia kupata mavuno yanayoridhisha.
Kwa upande wa wakulima pia wamemwelezaMkuu wa Mkoa huyo juu ya changamoto wanazokumbana nazo ikiwemo uhaba wa vitendea kazi pamoja na pembejeo za kilimo kuwa ndio kinawakwamisha kufanya kilimo chenye tija.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 komentar: