Haji Manara Aungana na Yanga


Afisa habari wa timu ya Simba SC, Haji Manara amekuwa miongoni mwa watu walioweza kuguswa na msiba uliomfika Nahodha wa Yanga SC, Nadir Haroub 'Cannavaro' leo wa kufiwa na mwanae na kumtaka awe mwenye moyo wa subra.

Manara amefunguka hayo kupitia ukurasa wake maalumu wa kijamii baada ya kupokea taarifa hizo za msiba wa Anwar aliyefariki katika hospitali ya Taifa Muhimbili leo asubuhi wakati akipatiwa matibabu ya maradhi yaliyokuwa yakimsumbua

"Pole sana Cannavaro kwa kufiwa na mtoto wako wa miezi miwili Anwar. Mimi binafsi, viongozi, wachezaji, benchi la ufundi, wanachama pamoja na mashabiki wa Simba tunaungana na Cannavaro katika kipindi hiki kigumu alichonacho yeye pamoja na familia yake kiujumla. Poleni wanayanga wote",amesema Manara.

Kwa upande mwingine, muandishi wa habari hii alipomtafuta Cannavaro kwa njia ya simu amesema japo kuwa yeye yupo njiani kurudi nchini akiwa anatokea Visiwa vya Shelisheli ameruhusu mwili wa marehemu mwanae kuzikwa leo (kuhifadhiwa).
Previous Post
Next Post

post written by:

0 komentar: