FAINALI za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17  zitafanyika katika Jiji la Dar es Salaam pekee mwakani.

Hayo yamesema leo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison George Mwakyembe katika mkutano wake na Waandishi wa Habari Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam leo.

Mwakyembe aliitisha mkutano na Wahariri na Habari kuzungumzia ziara ya Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Giovanni Vincenzo ‘Gianni’ Infantino aliyekuwa nchini kati ya Februari 21 na 23 kwa ajili ya mkutano maalum wa shirikisho hilo ulioshirikisha nchi 21, wakiwemo wenyeji Tanzania.

Mwakyembe amesema kwamba Rais wa Shirikisho la Afrika (CAF), Ahmad aliyeambatana na Infantino nchini ameridhia fainali za AFCON 2019 zifanyike katika Jiji la Dar es Salaam pekee.
Waziri Mwakyembe amesema kwamba infantino ambaye alipata fursa ya kukutana na Waziri Mkuu pia, Dk. Kassim Majaliwa kwa kiasi kikubwa amerejesha imani yake kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Mwakyembe amesema anaamini FIFA itaanza tena kuipa TFF ruzuku ya mwaka iliyopanda kutoka Sh. Milioni 500 kwa mwaka hadi Sh. Bilioni 2.7 baada ya kusitisha utaratibu huo tangu mwaka 2015.
Aidha, Mwakyembe amesema kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Joseph Magufuli naye ameishukuru FIFA kwa kufanyia semina yake Dar es Salaam mwaka huu.

Na kuhusu Zanzibar kurudishiwa uanachama wa FIFA, baada ya mazungumzo yaliyomuhusisha Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo wa Zanzibar, Rashid Juma, Rais Infantino amekiri kuyaona mazingira ya uepekee wa suala hilo na kuwataka waendelee kubadilishana mawazo
Share To:

msumbanews

Post A Comment: