Jina la mmea “mwarobaini” linatokana na imani kuwa mti huu una uwezo wa kutibu magonjwa yapatayo arobaini. Majani, mizizi na mbegu za mwarobaini vimekuwa vikitumiwa kama tiba kwa miaka maelfu katika nchi mbalimbali duniani kote.

Kwa jina la kitalamu Mwarobaini huitwa (Azadirachta indica) ni mti unaofahamika kwa uwezo wake wa kutibu magonjwa ya aina mbalimbali. Inaaminika kuwa mti huu umetoka huko India na Burma .

Mwarobaini hushamiri zaidi katika nchi za tropiki na una uwezo mkubwa wa kuhimili ukame. Nchini Tanzania, mti wa mwarobaini huweza kupatikana kwa urahisi kabisa katika maeneo mengi ya mijini na vijijini. Kwa hapa tanzania mimea hii inapatikana kwa wingi zaidi mkoa wa dodoma.

Yapo magonjwa ambayo mti huu umetumika kutibu ni pamoja na matatizo ya kusaga chakula tumboni, kisukari, kansa, magonjwa ya ngozi, malaria, ukungu (fungus), n.k. Matawi yake hutumiwa kama mswaki na magome yake hutumiwa kama dawa ya kusafisha meno.

Hatua za kuzingatia
Chukua majani mabichi ya mti wa mwarobaini na uyaweke kwenye sufuria.
Chukua sufuria yako yenye majani ya mti wa mwarobaini na uinjike kwenye jiko lenye moto wa wastani. Chukua mwiko wako na uanze kuyakoroga majani yako taratibu hadi yakauke bila kuungua.

Faida ya mwarobaini
Hutunza ngozi na kuponya baadhi ya magonjwa yatokanayo na maabukizi ya ngozi mwarobaini hutibu magonjwa mengi ya ngozi yanayoambukiza na yasiyoambukiza. Hutibu vidonda vya kuungua vilivyochunika

Matumizi
Kunywa kikombe kidogo cha chai kwa siku 21 utaona mabadiliko katika ngozi yako
Share To:

msumbanews

Post A Comment: