Mtu mmoja wilayani Mkalama Singida aliyefahamika kwa majina ya Mpanda Jumapili (35) auawa kwa kuchomwa kisu kifuani na Daudi Labani kwa ugomvi wa shilingi 4000 uliotokea kwenye michezo ya kubahatisha
Akiongea na eatv Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Deborah Magiligimba amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa chanzo cha kifo hicho ulikuwa ni ugomvi ulioanzia kwenye ugomvi mchezo wa kubahatisha. 
"Mtuhumiwa pamoja na marehemu walikuwa wanacheza mchezo wa kubahatisha katika mashine ya kichina kwa hiyo mzozo ulianzia maeneo hayo wakatoana nje na mtuhumiwa aliweza kumchoma kisu marehemu upande wa kushoto kufuani, alikimbizwa hospitali na mauti ulimkuta akiwa hospitali hivyo baada ya wananchi ambao walikuwa pale walipoona hilo tukio walimkamata huyo mtuhumiwa na kutoa taarifa kituo cha polisi lakini wakiwa wanaelekea kituoni lilijitokeza kundi jingine kwa nyuma likiwarushia mawe na fimbo na walipokaribia kituoni jiwe moja lilimpata huyo mtuhumiwa kichwani akaanguka hapo hapo" 
Kamanda aliendelea kutoa ufafanuzi kuwa 
"Baada ya yule mtuhumiwa kuanguka wale wananchi waliendelea kurusha mawe na kuharibu baadhi ya vitu katika kituo cha polisi na kuharibu taa nne na kuvunja madirisha mawili ya vioo ya kituo cha polisi, huyo mtuhumiwa mpaka sasa amelazwa hospitali akipatiwa matibabu kufuatia majeraha aliyopata kwa kipigo cha wananchi" alisema Deborah
Share To:

msumbanews

Post A Comment: