CHAMA cha Demaokrasia na Maendeleo (Chadema) kimekanusha taarifa inayosambaa mitandaoni kuwa wamejitoa kwenye uchaguzi mdogo wa ubunge kwa majimbo ya Kinondoni na Siha unaotarajiwa kufanyika kesho Jumamosi, Feb 17, 2018.

Akizungumza na Msumbanews.co.tz jioni Msemaji wa Chadema, Tumaini Makene,amesema taarifa hizo si za kweli na kwamba zimeandaliwa ili kuwapotosha wapiga kura.

Naye Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema:
“Kuna barua inasambazwa kwenye Mitandao kuwa CHADEMA imejitoa kwenye uchaguzi wa Majimbo ya Kinondoni na Siha, hizi ni propaganda dhaifu za waliokwishashindwa, wanafanya hivi kuwakatisha tamaa wapiga kura ili wasijitokeze kesho kupiga kura, wapuuzeni hao.

“Hawajui hata utaratibu kuwa ni mgombea tu ndiye mwenye haki ya kuandika barua ya kujitoa na si M/Kiti wa Chama.  Mbowe anafunga kampeni Kinondoni muda huu na mzee Lowassa anafunga Kampeni Siha muda huu huu.”



Share To:

msumbanews

Post A Comment: