Image result for picha chadema
Mwenyekiti wa Chadema  Freeman Mbowe ametangaza kusitishwa  kwa kampeni ili kujumuika katika mazishi ya Kingunge Ngombale Mwiru.
Hayo aliyasema  kwenye kampeni za kumnadi mgombea ubunge wa jimbo la Kinondoni Salum Mwalimu kwenye viwanja vya Kinondoni manyanya.
Mbowe alisema Kingunge ni mtu alifanya mengi kwenye taifa hili kutokana na uadilifu wake na kesho kwa pamoja tunamsindikiza.
"Mzee Kingunge ni mtu mwadilifu amefanya mengi kwenye taifa hili alikuwa CCM na baadaye Chadema kesho tutasitisha kampeni ili kushiriki maziko" amesema Mbowe.
Naye  mgombea ubunge  Mwalimu amesema vipaumbele vyake ni vitatu ila atakapochaguliwa ataanza na elimu pamoja na afya.
"Najua kata nyingi hazina vituo vya afya wala shule za kata mtakaponichagua kipaumbele changu cha kwanza nitahakikisha  kila kata inakuwa na kituo cha afya na shule ya sekondari" alisema Mwalimu.

Share To:

Post A Comment: