Friday, 16 February 2018

CHADEMA wapigwa mabomu ya machozi Kinondoni


Jeshi la Polisi mkoa wa kipolisi wa Kinondoni limetumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa (CHADEMA) waliokuwa wakiandamana kuelekea katika ofisi ya Mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni.

Wafuasi hao wa CHADEMA waliamua kufanya maamuzi ya kwenda kwa Mkurugenzi wa Uchaguzi kwa kile walichosema kuwa mpka leo majira ya saa 12 jioni  Mawakala wao walikuwa hajapewa barua za kuwatambulisha licha ya kuwa waliapishwa toka siku tano zilizopita. 

Mbowe amesema jana walipata nafasi ya kuongea na Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi NEC na kuwa aliwaahidi kuwa mpaka leo Februari 16, 2018 mapema sana tatizo hilo lingekuwa limetatuliwa. 

Baada ya kumaliza kwa mkutano wao wa mwisho leo Mwenyekiti wa CHEDEMA Freeman Mbowe aliwaambia wanachama wao pamoja na viongozi wengine waongozane kuelekea ofisi ya Mkurugenzi wa Uchaguzi ili wakapate haki yao hiyo kwa kuwa wanatambua kuwa Mkurugenzi huenda yupo busy na mambo mengine.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: