Cannavaro -"Tupo tayari kwa mapambano"


Nahodha wa Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro' amefunguka na kudai kikosi chao kimejipanga vizuri katika mchezo wa marudiano wa ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya St. Louis unaotarajiwa kufanyika kesho (Jumatano)

Cannavaro amebainisha hayo leo kupitia ukurasa maalumu wa timu hiyo muda mchache walipokuwa wamemaliza kufanya mazoezi ya mwisho kabla hawajawavaa wapinzani wao na kusema watahakikisha watautimia mchezo wao vizuri ili waweze kuendelea kushiriki katika michuano hiyo.

"Tunashukuru Mungu tumemaliza salama mazoezi na kila mchezaji anahamu ya kucheza mechi ya kesho. Tunawaomba watanzania kwa ujumla na Afrika watuombee dua ili tuweze kufanya vizuri mchezo wetu wa dhidi ya St.Louis. Sisi ahadi yetu ni kufanya vizuri ili tuweze kuendelea kushiriki mashindano ya kimataifa, morali ya wachezaji iko vizuri na tupo teyari kwa mapambano", amesema Cannavaro.
Timu ya Yanga katika mchezo wake uliyopita dhidi ya St.Lousi ya kutokea Shelisheli walifanikiwa kutoka vifua mbele kwa kupata ushindi wa bao 1-0 mchezo uliyochezwa katika dimba la Taifa Jijini Dar es Salaam. 
Previous Post
Next Post

post written by:

0 komentar: