Saturday, 17 February 2018

Breaking News : Mwalimu Akamatwa na Polisi
Mgombea ubunge wa Chadema jimbo la Kinondoni, Salum Mwalimu amekamatwa muda huu na polisi katika kituo cha kupigia kura cha Idrisa kata ya Magomeni.
Muda mfupi uliopita baadhi ya wananchi wa kata hiyo wamedai kuwa katika kituo hicho kuna mtu ametoroka na sanduku lenye kura, baadaye kukamatwa na polisi akiwa amelibeba sanduku hilo.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa alipoulizwa kuhusu kukamatwa kwa Mwalimu amesema kuwa hana taarifa zozote.

Baada ya kufikishwa kituo cha polisi Magomeni, Mwalimu aliingizwa ndani na kukaa takribani robo saa na kuachiwa na muda huu anaelekea ofisi za kanda za Chadema kuzungumza na waandishi wa habari.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: