Monday, 26 February 2018

Bocco Akabidhiwa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi January

Wakati Simba SC ikitawala vema msimamo wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara kwa kujikusanyia jumla ya alama 44 mpaka sasa wakati huo huo mshambuliaji wake, John Bocco anajishindia tuzo ya mchezaji bora.
Bocco amejishindia tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Januari hii leo wakati wa mchezo wa timu yake ya Simba SC dhidi ya Mbao FC ya jijini Mwanza.
Wakati mshambuliaji huyo akitwaa tuzo hiyo ya mwezi, timu yake ya Simba SC hii leo wameweza kuifunga timu ya Mbao FC kwa jumla ya mabao 5 – 0  bila huruma mchezo wa ligi kuu soka Tanzania Bara uliyopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: