Wednesday, 21 February 2018

Bao la nyumbani laibeba Yanga SC dhidi ya St Louis


Mabingwa wa tetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara klabu ya Young Afrcans imefanikiwa kusonga mbele katika michuano ya klabu bingwa Afrika baada ya kulazimishwa sare ya bao 1 – 1  dhidi ya St Louis huko Shelisheli
Yanga SC imepata bao hilo kupitia kwa mchezaji wake Ibrahim Ajib katika kipindi cha kwanza wakati St Louis wakipata bao lake kipindi cha pili.
Yanga SC imefanikiwa kusonga mbele baada ya kujikusanyia jumla ya mabao 2 – 1 baada ya mchezo wa awali kuibuka na ushindi mwembamba wa bao 1 -0 uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

No comments:

Post a comment