Thursday, 22 February 2018

Baadhi ya Wanafunzi wapoteza fahamu baada ya mwili wa Akwilina kuwasili

Vilio, simanzi na kupoteza fahamu kwa baadhi ya wanafunzi ni baadhi ya matukio ya huzuni yanayojitokeza katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), baada ya kuwasili mwili wa aliyekuwa mwanafunzi wa chuo hicho, Akwilina Akwiline.

Mwili wa mwanafunzi huyo unaagwa leo, Februari 22, 2018 katika viwanja vya chuo hicho.

Wanafunzi zaidi ya wanne aliokuwa akisoma nao Akwilina chuoni hapo ni kama hawaamini baada ya kushuhudia jeneza lenye mwili wake, huku wengine wakipoteza fahamu na kupewa huduma ya kwanza na Shirika la Msalaba Mwekundu.

Viongozi waliofika mpaka sasa katika viwanja vya NIT ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi; Waziri wa Elimu, Profesa Joyce Ndalichako; Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni; Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa na Mbunge wa Kibamba (Chadema), John Mnyika.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: