Baada ya kumwagwa na Zari, Diamond atangaza neema hii Kenya


Wakati stori ya Diamond kutemwa na Zari The Bosslady ikishika kasi, bosi huyo wa WCB ametangaza neema mpya kwa wasanii wenye vipaji nchini Kenya.

Diamond kupitia mtandao wa Instagram, amethibitisha kuwa mwaka huu wanatarajia kufungua tawi jipya la WCB ambalo ni maalum kwa ajili ya kusaidia kuinua vipaji vya wasanii wa mitaani ambao hawajapata nafasi.
Kupitia mtandao huo, Diamond ameandika:
Kama unavyofaham mwaka huu @wcb_wasafi tunafungua Tawi jipya nchini Kenya, Maalum kwajili ya kuendelea kunyanyua vijana wenzetu wenye Vipaji tokea mtaani.. tafadhali nisaidie kuwatag vijana wote wenye Vipaji kenya, akianziwa na Huyu…)
Previous Post
Next Post

post written by:

0 komentar: