Saturday, 24 February 2018

Arusha Press Club watuma salamu za Rambirambi msiba wa Hassan Simba


Uongozi wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Arusha (Arusha Press Club) na waandishi wa habari kwa ujumla mkoani Arusha umepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa ya kifo  cha Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Mtwara  Hassan Simba ambaye amefariki dunia leo Februari 24,2018 alipokuwa akipatiwa matibabu katika hospitali ya Temeke Jijini Dar es salaam.

APC inawapa pole ndugu jamaa, marafiki, wanachama wa Mtwara Press Club,UTPC, MCT na waandishi wa habari wote nchini. Hakika tasnia ya habari imepoteza mtu muhimu sana ambaye mchango wake bado ulikuwa unahitaji hasa ktk kipindi hiki cha mpito kuelekea kwenye utekelezwaji wa sheria mpya ya huduma ya habari.

Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake  lihimidiwe

Claud Gwandu - Mwenyekiti Arusha Press Club (APC)
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: