Mjasiriamali anayefanya biashara ya kuuza magazeti katika kituo cha Sadala wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, Irene Shao amejikuta akipewa adhabu ya kupiga deki katika ofisi ya mtendaji wa kata kwa miezi mitatu baada ya kushindwa kujitokeza siku ya kufanya usafi.
Akieleza kwa hisia juu ya adhabu hiyo, Bi. Shao  amesema amepewa adhabu hiyo baada ya kushindwa kwenda kufanya usafi siku ya Alhamisi iliyokuwa imebadilishwa kutoka siku iliyozoeleka ya Jumamosi ya mwisho wa mwezi ambayo ni siku ya kitaifa kufanya usafi..
Shayo amesema siku hiyo ya usafi ya Alhamisi aliendelea na biashara yake kwani hakujua kama ratiba imebadilishwa na uongozi wa kata ya Masama Kusini, ndipo baadaye alipokamatwa na kupewa adhabu hiyo.
Sikuwa na taarifa za kubadilika kwa siku ya usafi, siku hiyo nikaendelea na majukumu yangu ya kufuata magazeti mjini Moshi na niliporudi nikakuta tayari usafi umefanyika hivyo mtendaji akaniambia nimekaidi agizo,”amesema Bi. Shao kwenye mahojiano yake na gazeti la Mwananchi.
Hata hivyo, Kaimu Mkurugezi wa Wilaya ya Hai, Edward Ntakiliho amezungumzia suala hilo kwa kusema kuwa  siku ya usafi ni Jumamosi ya mwisho wa mwezi kama ilivyotangazwa na serikali na adhabu ya kwa mtu yeyote atakayekiuka ni faini ya Tsh 50,000/= au kifungo cha mwaka mmoja
Share To:

msumbanews

Post A Comment: