ANAANDIKA MBUNGE ANTHONY MAVUNDE


Leo nimefanya mkutano na wananchi wa Kata ya Nzuguni kujadili Changamoto mbalimbali katika kata hiyo lakini kubwa ikiwa ni kushughulikia changamoto ya uharibifu wa miundombinu ya barabara uliotokana na mvua zilizonyesha.

Niliongozana na Meneja wa Wilaya wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini(TARURA) Eng Kilembe ambapo tumekubaliana kimsingi kwamba zoezi la ukarabati wa barabara lianze wiki ijayo ili kuzifanya barabara hizo zipitike kwa urahisi na tayari Mkandarasi ameshapatikana kwa ajili ya utatuzi wa kero hii.

Kero ya Barabara Nzuguni imekuwa kubwa kiasi cha kusababisha adha kubwa kwa wasafiri wa eneo husika.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 komentar: