Na Ferdinand Shayo

Aliyekuwa Mgombea Ubunge kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CDM) jimbo la Siha Mkoani Kilimanjaro Bw elvis Mosi amesema kuwa ana mpango wa kufungua kesi mahakamani kupinga matokeo  ya uchaguzi yaliyompa ushindi Dr Godwin Mollel wa CCM kwa madai kuwa taratibu na kanuni za uchaguzi zilikiukwa hivyo  anatarajia kulifikisha suala hilo mahakamani.

Bw Mosi ambaye alipata kura 5905 dhidi ya kura 25611 za Dr Mollel amesema, wanakusanya ushahidi wa kutosha ambao utaiwezesha mahakama kutengua matokeo hayo na uchaguzi kurudiwa.

Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake sanya juu bw mosi amezitaja baadhi ya taratibu hizo kuwa ni pamoja na kubadilisha matokeo ya kura zake katika vituo na kupewa dr mollel jambo ambalo lilimfanya asisaini fomu za matokeo..insert ya bw elvis mosi mgombea ubunge wa ccm jimbo la siha.

Afisa 0ganizesheni wa Halmashauri na serikali za mitaa wa cdm kanda ya kaskazini Bw Ndonde Totinan amesema, matokeo ya kata 11 kati ya 17 ya jimbo hilo yana utata mkubwa ambao hawaridhiki nao na idadi ya kura zilizopigwa ziliongezwa katika baadhi ya vituo....insert ya bw ndonde totinan afisa ognizesheni wa CMD kanda ya Kaskazini.

Naye Mgombea wa Ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CUF Bw .Tumsifuel Mwanri ambaye hakusaini fomu za matokeo amesema, uchaguzi huo haukuwa huru na ulijaa ukiukwaji mkubwa wa haki za binaadam.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: