Friday, 23 February 2018

Akwelina alikuwa anamsomesha mdogo wake

Binti Akwelina Akwelini aliyepigwa risasi Februari 16, 2018 na kuzikwa leo Februari 23, 2018 Rombo mkoani Kilimanjaro imebainika kuwa binti huyo kupitia fedha ya mkopo ambayo alikuwa akipewa na serikali alikuwa anaitumia kumsomesha mdogo wake wa kike
Akiongea leo wakati wa mazishi ya Akwelina Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa. Joyce Ndalichako amesema kuwa ameguswa sana na jambo hilo hivyo ameamua kumchukua huyo binti na kumsomesha yeye. 
"Binti huyu ambaye tumempumzisha kwenye nyumba yake ya milele alikuwa anapambana katika kusaka elimu ili aweze kuikwamua familia yake nimesikitika pia kuona kwamba pamoja na fedha zile ambazo Akwelina alikuwa anapata kwa ajili ya yeye kujikimu lakini alikuwa anatumia fedha hizo hizo kumsaidia mdogo wake Angela ambaye yupo kidato cha tatu naomba nisema kwamba huyo binti Angela nitamchukua kwa sababu natambua na kuthamini elimu hivyo nitahakikisha kwamba namsomesha mpaka uwezo wake na ndoto zake zitakapofikia" alisema Ndalichako 
Aidha Ndalichako aliwaomba watu kuungana katika msiba huo na kuwataka kudumisha amani na mshikamano na kudai kuwa mambo yote yanayotokea duniani Mungu ndiye anakuwa na makusudio yake. 
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: