bao1

Baadhi ya Watumishi wa Umma wakiendelea kupata huduma ya usajili na Utambuzi katika viwanja vya Sabasaba ambako maonesho ya kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru yanafanyika. Wakati wa zoezi hilo mbali na kjaza fomu za maombi ya Vitambulisho, watumishi hao wamepata fursa ya kupigwa Picha, kuchukuliwa alama kumi (10) za vidole pamoja na saini ya Kielektroniki na hivyo kuwa wamekamilisha taratibu zote muhimu za usajili

bao2

Mmoja wa Watumishi akiendelea na taratibu za usajili na kuchukuliwa alama za kibaiolojia wakati wa usajili watumishi wa Umma, zoezi linaloendelea mkoani Simiyu

bao3

Mmoja wa Maafisa Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa ofisi ya Wilaya ya Bariadi (mwemye kofia nyeupe), akiendelea kuingiza taarifa za mmoja wa Watumishi wa Umma aliyejitokeza kusajiliwa wakati zoezi la Usajili watumishi wa Umma likiendelea mkoani Simiyu. Wengine waliomzunguka ni Watumishi kutoka Idara, Taasisi na Wizara za Serikali wakiendelea kusubiria huduma hiyo

bao4

Akiweka saini ya kielektroniki kwenye kifaa maalumu cha kukusanya taarifa wakati wa zoezi la Usajili ni mmoja wa maafisa afya katika Mkoa wa Simuyu ambaye alikuwa miongoni mwa watumishi waliojitikeza kusajiliwa Vitambulisho vya Taifa sambamba na maadhimisho ya kilele cha sherehe za Mwenge

Watumishi wa Umma mkoani Simiyu; wamekuwa miongoni mwa watumishi waliojitokeza kwa wingi kusajiliwa Vitambulisho vya Taifa katika zoezi linaloendelea kote nchini, pamoja na kusherehekea kilele cha mbio za Mwenye wa Uhuru zinazoadhimishwa kitaifa mkoani Simuyu. Kilele cha sherehe hizo ni Octoba 14,2016 sherehe zitakazoambatana na kumbukumbu ya Hayati Baba wa Taifa; Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Miongoni mwa watumishi wanaoendelea na Usajili  katika mabanda maalumu ya maonyesho mkoai humo; ni Walimu na watumishi wengine kutoka sekta ya Afya, WIzara, Wakala  na Taasisi za Serikali

Wakizungumza wakati zoezi hilo likiendelea; mbali na kupongeza  elimu kwa umma inayoendelea kuhusu namna zoezi la Usajili ili na Utambuzi litakavyoendeshwa nchi nzima, watumishi hao wamepongeza jitihada kubwa za Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dr. John Pombe Magufuli kwa kutofumbia macho matatizo ya watumishi na hasa jitihada zake katika kupambana na watumishi hewa.

“ iwapo kweli mfumo huu utatumika vile tunavyoelezwa kwa hakika shughuli za utendaji Serikalini zitaboreshwa sana hususani masuala yanayohusu maslahi ya watumishi na kuondokana kabisa na watumishi wachache ambao kwa udanganyifu wao wamepelekea sisi watumishi wa Umma kutothaminiwa na jamii” walisisitiza baadhi ya watumishi waliozungumza na NIDA wakati zoezi hilo likiendelea

Kwa upande wa wananchi wengi wameonyesha kuwa na uelewa wa kutosha kuhusu faida za kuwa na Vitambulisho vya Taifa, na mfumo wa kielektroniki utakaounganishwa na mifumo mingine ya Serikali ingawa baadhi wamesisitiza bado elimu kwa umma kuhusu Vitambulisho inahitajika hususani kwa wananchi walioko vijijini

Sherehe za mwaka huu za kilele cha mbio za Mwenge Kitaifa, zimekwenda sambamba na maonyesho ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na  Taasisi, Masharika na Wakala za Serikali; katika kuongeza uelewa na ushiriki wa wananchi katika shughuli za maendeleo

Share To:

msumbanews

Post A Comment: